Nilianzisha hii station tangu nilipokuwa form 1 wakati nilisoma physics kutoka shule.
Nimechukuwa muda ku-establish na kwa miaka miwili nilitumia battery kui-run
Ku-stopisha mathe kuingia kwa keja yangu imekuwa ngumu, hata hajui mi hufanya nini. Ye hufikiri mi huwa always nasoma ama naunda maredio za ma-neighbours ili nipate dooh kidogo kidogo.
Neighbour wangu alinipea TV yake ya black and white ilipoharibika na kununuwa mpya ya color juu hawakufikiri ingetengenezwa. Nilipata spares za kuunda Shujaaz FM na kutoka scraps za radio zingine. Parts zingine niliunda, kama umbrella ya mathe ikawa aerial na zingine nikanunua na dooh nilizopata.
Chief aliponipa job ya ku-fix PA na aliponilipa 200/=, nilionunua micro chip iliyokuwa important kwenda on air.
Niki-tune pole pole, naweza pata kuskika kutoka frequency any na ku-air kwa dakika kadhaa.
Si kwa muda mrefu, juu naweza trace-iwa na basi station kufungwa.
Kabla nipatwe, mimi ni Shujaaz FM- Shujaa wa ku-pirate mahewa!!!
Sawa, uliskia, hapana?
Ile youth group ilikuja kuitisha pesa ya security, na juu ni Christmas, wakaniitisha double malipo ya kawaida.
Lakini kile kibaya ni kuwa mabeste wangu wamejoin hiyo group! Unajuwa tulisoma na wao kutoka prima mpaka seko, halafu wana-come kuniitisha doo kama hawanijui!?
Siwezi wa-blame, ni vile hakuna ma-jobs huku.Lakini staki kufanya kama wao. Sitawahi join ma-gangs na kulipa dooh za security yao
Nimekuwa nikifikiria ni nini naweza fanya na Shujaaz FM, lakini sasa nimejua
Nitatafuta ma jobs na ma-ideas za hawa machali walio kwa gangs. Nitatafuta njia za kuwasaidia kupata dooh na kuanzisha maisha poa badala ya ku-force wasee kutoa dooh
Nitumie SMS kwa nambari 3008 ili kuniuliza juu ya ideas zile nimewapea ama tuma habari yako kupitia hii website. Wale watakuwa na ma-ideas poa zaidi, nitawapigia simu na kuwa-interview kwa hii show.


